Shirika la ndege la Etihad, ndege rasmi ya
taifa za Falme za kiarabu, imefanikiwa kuchangisha kiasi cha dirhams milioni
moja kwa ajili ya kusaidia kampeni ya “we care Yemen” hii ikiwa ni pamoja na
kusaidia kukarabati shule mbili nchini Kenya kama sehemu ya mpango wa kila
mwaka wa shirika hili la ndege la kuchangisha fedha kwa kushirikiana na shirika
la Red Crescent kutoka nchi ya Falme za kiarabu pia.
Mchango huu ulitangazwa wakati wa kufunga
sherehe za kombe la dunia la mashirika ya ndege kwa upande wa mpira wa miguu na
tamasha la vyakula na fashion, vyote vikiwa vimeandaliwa na kamati ya michezo
na jamii ya shirika la Etihad, lilofanyika ukumbi wa kimataifa wa Al Forsan.
Timu za soka kutoka mashirika 28 ya anga na
ndege yalishiriki kwenye tamasha hilo lilokuwa na mashindano mbalimbali
yakiwemo uchoraji wa henna, burudani ya mziki, ballet and michuano ya mavazi.
Shirika la Etihad lilitoa zawadi kemkem ikiwepo safari kwenda kenya kwa mshindi
wakwanza na wapili.
Makamu wa raisi wa shirika la Etihad masuala
ya siasa za anga, Khaled Al Mehairbi, anayetumikia kama mwenyekiti wa kamati ya
michezo na jamii, alisema “ Kama shirika la ndege la taifa ya Falme za kiarabu,
tunapenda kuthibitisha dhamira yetu kwa jamii na kujitolea kwa wale wenye
uhitaji. Tunayo furaha kushirikiana na
UAE Red Crescent katika kutumikia and kusaidia jamii husika”.
“Tungependa kutoa shukrani za dhati pia kwa
wageni, wadhamini and wauzaji walioshiriki kwa mioyo yao ya dhati kuchangia
kampeni hii kwa mwaka 2015 ili kusaidia wale wenye uhitaji. Kwa pamoja tumetoa
mwanga wa matumaini na nafasi ya maisha bora ya baadae kwa kaka na dada zetu waliopo Yemen na Kenya”
Sherehe za ufunguzi ziliongozwa na bendi ya taifa
ya vijana wasio na uwezo wa kusikia. Tamasha hilo lilishuhudia burudani kutoka
kwa “Sala the Entertainer”, mshindi wa mashindano ya X Factor 2015, na msanii
kutoka Marekani, Dynasty. Burudani kutoka kikundi cha watoto waliocheza
“Ballet” pia ilikuwa kivutio kikubwa katika tamasha hilo.
Michango ya hisani kwa Yemen ilikusanywa
kupitia matukio mbalimbali ikiwemo mchango wa “Etihad gGuest Miles Online”,
Kupitia timu ya soka ya Etihad, Mauzo ya vitu kutoka Etihad, mchango wa vifaa
vya shule na mabegi mapya kwenda kwa watoto nchini Yemen kupitia wafanyakazi wa
shirika la ndege la Etihad, na mchango wa fedha taslimu kwenye visanduku vya
Emirates Red Crescent.
Mipango ya shirika kusaidia kampeni ya “We
Care Yemen” na Kenya ni sehemu ya makubaliano ya awali juu ya ushirikiano wa
kiubinadamu na kijamii baina ya shirika la ndege la Etihad na Emirates Red
Crescent.
Tukio hili la kijamii lilihudhuriwa na
mheshimiwa Khadija Issa Yusuf, Balozi wa kenya kwa nchi ya Falme za kiarabu,
Bw. Humaid R Al-Shamsi, Naibu katibu mkuu kwa misaada ya kimataifa kutoka
shirika la Emirates Red Crescent, Dr. Khalwa Salem Al Saaedi, mwakilishi wa
Rais wa shirika la kimataifa la muungano wanawake na afya.
Wengine waliohuduria walikuwa katibu mkuu,
Mheshimiwa Mariam Saif Al Qubasi, Mkuu wa sekta ya mahitaji maalumu kutoka
Zayed Higher Organization (ZHO), Hamad Alhosani, Mtendaji mkuu wa TCA Abu
Dhabi, na Mohammad Ali Khilji, meneja mkuu wa Axiom UAE.
Shirika la ndege la Etihad liliwakilishwa na
Peter Baumgartner, Afisa mkuu wa biashara, Khaled Al Mehairbi, Makamu wa Rais masuala ya
siasa za anga, Ali Al Shamsi, Makamu wa Rais Abu Dhabi Hub, Oliver Iffert, Makamu
wa rais uendeshaji masuala ya Ndege, na Geert Boven, Makamu wa Rais huduma wa
Uwanja wa ndege.
Mwaka 2015, shirika la ndege la Etihad
liliweza kuchangisha Etihad Guest miles, bidhaa za msaada na fedha taslimu
yenye thamani ya zaidi ya dirhams milioni tatu.
Tamasha hili la siku mbili lilifanyika kwa
kushirikiana na Emirates Red Crescent, baraza la michezo la Abu Dhabi, vyombo
vya habari vya Abu Dhabi, ukumbi wa kimataifa wa michezo wa Al Forsan, Hoteli
za Time, Shirika la wanawake la Joyful, kampuni ya maji ya Al Ain, Bottega
Verde, Dusit Thani Abu Dhabi, Axiom UAE, Sebamed, Fusion Arts, Gabs, Pierre
Fabre, Hoteli za Yas Viceroy, Novotel Al Bustan, Holiday Inn Abu Dhabi, Hoteli
za One to One, Yas Waterworld, Maabara za dawa za Al Borg Medical, Al Jaber
Optical, Mikura Pearls, Conrad Dubai, Absolute Dry, Zartux, and Hoteli ya Tilal
Liwa.
- Mwisho-
Kuhusu Shirika la Ndege la Etihad
Shirika la Ndege la Etihad
lilianza shughuli zake mnamo mwaka 2003 na hadi kufikia mwaka 2014, ilikuwa
limeshabeba abiria takriban milioni 14.8. Kutoka makao makuu yake huko Abu
Dhabi, shirika hili linasafiri au limetangaza mipango ya kuhudumia wasafiri na
mizigo kutoka vituo 116 huko Mahariki ya kati, Afrika, Ulaya, Asia, Australia
na nchi za Americas. Shirika lina ndege aina ya Airbus na Boeing takriban 120,
Zaidi ya ndege 200 zikiwa zimewekea oda, zikiwemo Boeing 787s 66, Boeing 777Xs
25, Airbus A350s 62 na Airbus A380s tano.
Shirika la Etihad pia limewekeza
katkia AirBerlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Jet Airways , Virgin
Australia, pamoja na shirika lenye makazi Uswiss Darwin Airline, likifanya
biashara kama Etihad Regional. Shirika la Ethihad, sambamba na airberlin, Air Serbia, Air Seychelles,
Alitalia, Etihad Regional, Jet Airways na NIKI, pia hushiriki pamoja nkwatika
washirika wa Etihad Airways, brand mpya inayowaleta kwa pamoja mashirika
mengine ya ndege yenye uelewa sawa ili kutoa huduma bora zaidi kwa wateja,
kuwapa wateja ratiba nzuri Zaidi na kuwazawadia wateja wakudumu.kwa maelezo
Zaidi, tafadhali tembelea :www.etihad.com
No comments:
Post a Comment