Masogange alipost kipimo cha ujauzito kwenye page yake ya Instagram, post iliyoibua mjadala mkubwa Nigeria na Tanzania na kuacha swali kubwa vichwani mwa watu, “Agnes ana ujauzito wa Davido?!”
Baada ya ukimya wa siku kadhaa, Davido aliamua azungumze na kuweka mambo sawa ili kusitisha uvumi unaosambaa juu yake na Agnes Masogange… kupitia page yake ya Twitter, Davido alipost tweets kadhaa huku akidai tetesi hizo zimemuumiza zaidi baada ya mrembo Masogange kumuendea hewani staa huyo kwa uchungu na kudai uhusiano wake na mpenzi wake upo matatani kutokana na uvumi huo.
Haya ndio majibu ya Davido kuhusu uvumi wa Agnes Masogange kubeba ujauzito wake.
"TBH sijali Blogs zinaandika nini Ukweli au Uongo lakini pale ambapo mtu ananipigia kutoka nchini nyingine analia… Kuhusu mchumba wake kuona taarifa za uongo na anakaribia kuondoka na kumuacha… na machungu!! Haya ni maisha ya watu ambayo nyie watu mnayachezea, mpaka kitu cha ajabu kitokee ndipo watu watakapojiona wajinga…Tafadhali acheni, hii sio haki kwa Agnes na mpenzi wake, waache waishi na kupata mtoto wao kwa amani… Nimetajwa kama miongoni mwa watu wenye ushawishi mkubwa kwa mwaka 2015 na FORBES AFRICA kwanini msiisambaze hii...Lakini taarifa yoyote mbaya mtaishambulia na kuiandika! Msinichukulie vibaya, kama ni taarifa za ukweli basi hakuna ubaya wowote… Lakini kwanini msambaze uongo!!! Tunaishi kwenye dunia iliyovurugwa!! Hii social media tunaitumia kwa level nyingine...Siku moja mtakuja kuandika ujinga kuhusu mtu ambaye haiwezi hii presha na mtaona kitakachotokea!!!
No comments:
Post a Comment