Na. Julius Mtatiro
(TAHADHARI:
Kama una Jazba usichangie POST hii - Utakufa kwa Presha Bure, Posti hii
inaweza kuibua hisia kali, hofu, wasiwasi na majuto ikiwa unakubaliana
na maoni haya au unayapinga na ikiwa mgombea wako amegongwa mahali hapa
au ameparazwa, jadili hoja wala usimguse mtoa hoja)
Ndugu zangu,
Jana
Chama Cha Mapinduzi kimetoa orodha ya wagombea wake nchi nzima. Katika
orodha hiyo kuna watuhumiwa wengi tu wa masuala ya ufisadi, kuna
watuhumiwa wengi wa rushwa na wengine walikamatwa na kuhojiwa na
TAKUKURU, kwa kifupi kuna watuhumiwa kibao sana.
Lakini kubwa kuliko
yote USHAHIDI WA WAZI unaonesha kuwa hakuna mgombea hata mmoja wa CCM
anaweza kupita kwenye kura ya maoni nchi nzima bila kutoa rushwa kubwa
na ndogo, kwa wapiga kura wa kawaida na kwa viongozi wanaosimamia
uchaguzi. Nina marafiki zangu wengi tu wameshinda na kushindwa kwenye
kura za maoni ndani ya CCM, kila mmoja (aliyeshinda na aliyeshindwa)
wanasema kuwa PESA ndiyo inaamua nani hasa apitishwe ndani ya CCM.
Leo nataka kumuuliza ndugu yangu Humphrey Polepole
na aje hapa anijibu kwa hoja. Je, msimamo na mtizamo wake juu ya rushwa
ndani ya CCM uko namna gani? Nilipofuatilia mjadala kati yake na
Mchungaji Msigwa nilimuona Polepole akisisitiza kuwa kiongozi
akishatuhumiwa tu anapoteza political legitimacy ya kuwa kiongozi kwa
sababu anakuwa amepoteza "moral authority" (mamlaka ya kimaadili).
Polepole
amesisistiza kuwa Lowassa ni mtuhumiwa mkubwa wa ufisadi hasa kwenye
eneo la RICHMOND na kwamba hawezi kumuunga mkono, katika hilo
nakubaliana naye. Lakini pia nilitaraji Polepole atueleze kuwa Magufuli
pia ni mtuhumiwa mkubwa wa ufisadi na hasa akihusishwa na uuzaji holela
wa nyumba za serikali kwa manufaa binafsi na kuwapatia ndugu zake nyumba
nyingine zenye thamani kubwa.
Kama kutuhumiwa tu kwa masuala ya
kuvunja maadili kunamfanya mtu anyimwe haki ya kuwa kiongozi basi mwaka
huu tumeingizwa chaka na CCM na UKAWA! Kwamba vyama vyote vimesimamisha
wagombea ambao ni watuhumiwa wa ufisadi lakini hakuna mmoja kati yao
aliyewahi kuthibitishwa kwamba amekula pesa ngapi kwenye ufisadi huo.
Polepole
alikwenda mbali zaidi na kutoa sharti kubwa kwa uongozi wa juu wa CCM,
kwamba uongozi huo ukate wabunge wote ambao wana tuhuma au wamepita kwa
njia ya rushwa. Kwa bahati mbaya sana watuhumiwa wote wa ufisadi na
rushwa ndani ya CCM wamerejeshwa kugombea ubunge na nyadhifa zingine,
kina Andrew Chenge a.k.a Vijisenti, kina Prof. Tibaijuka a.k.a Hela ya
Mboga n.k. Kuna watuhumiwa wengine wa utoaji rushwa wakati wa kura za
maoni za CCM ambao walikamatwa na TAKUKURU na kuhojiwa, wote hawa
wameshapoteza MORAL AUTHORITY na POLITICAL LEGITIMACY!
Polepole
njoo usaidie kueleza watanzania nini ni mtizamo wako juu ya uchaguzi huu
ambao CCM imesimamisha mgombea urais ambaye ni mtuhumiwa namba moja wa
ufisadi wa UUZAJI WA NYUMBA ZA SERIKALI na UKAWA imemsimamisha mgombea
ambaye ni mtuhumiwa wa ufisadi wa RICHMOND. Njoo utueleze msimamo wako
juu ya uchaguzi ambao CCM imesimamisha zaidi ya robo tatu ya wabunge
ambao ni watuhumiwa wa ufisadi mkubwa na utoaji rushwa wa wazi kwenye
kura ya maoni dhidi ya UKAWA ambayo imesimamisha takribani zaidi ya ROBO
TATU ya wabunge ambao hawajawahi kujihusisha na ufisadi wala kutoa
rushwa kwenye kura za maoni za ndani ya vyama.
Na mwisho njoo
utueleze tatizo la Rushwa na Ufisadi ni la kimfumo zaidi au ni la mtu?
Njoo utueleze kuwa ni nani yuko kwenye nafasi nzuri ya kupambana na
ufisadi, Magufuli ambaye yumo bado ndani ya CCM au Lowassa ambaye yuko
nje ya CCM.
Njoo utueleze ni nani anaweza kupambana na ufisadi,
ni Magufuli Mtuhumiwa wa Ufisadi wa Nyumba za Serikali ambaye
amezungukwa na robo tatu ya wabunge waliotumia rushwa na uvunjaji wa
maadili kupita kwenye kura za maoni au ni Edward Lowassa mtuhumiwa wa
Ufisadi wa Richmond ambaye amezungukwa na wabunge waadilifu na wazalendo
waliopita kwenye kura za maoni bila kuhonga wala kutoa rushwa nikiwemo
mimi Mtatiro.
Na je baada ya CCM kuwapitisha watuhumiwa wa rushwa
lukuki kugombea ubunge kwenye kampeni za mwaka huu bado utakipigia debe
chama chako CCM?
Wala jazba hazihitajiki katika kujadili, tunahitaji
hoja kwa wachangiaji wote, tusiwe wanafiki, kama unakula Nguruwe hebu
kunywa na mchuzi wake, huwezo kujidai huli nguruwe huku unakunywa mchuzi
wake "daily
No comments:
Post a Comment