Msanii wa Bongo Fleva,Nuh Mziwanda amemkana tena staa wa Bongo
Movie,Wema Sepetu kuwa hajawahi kumtongoza na sauti iliyorekodiwa kwenye
simu akimtongoza mwigizaji huyo siyo yake.
Akizungumza kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM,alipokuwa akiachia
ngoma yake mpya iitwayo ‘Hadithi’ alisema kuwa Wema hakuwa na nia nzuri
na penzi lake na Shilole na alitaka kuwagombanisha na mpenzi wake huyo.
Sijawahi kumtongoza Wema na hakuwa na nia nzuri na penzi langu na
Shilole alitaka kutugombanisha na nasisitiza ile sauti haikuwa yangu,’’alisema Nuh Mziwanda

No comments:
Post a Comment