Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundega akiongea na wanahabari (hawapo pichani).
Kamati
inayosimamia mashindano ya Miss Tanzania Lino International Agency
imepata Mwenyekiti na wajumbe wapya watakaoandaa, kuratibu na kusimamia
mashindano ya urembo ya Miss Tanzania.
Akiwatambulisha wajumbe
hao mbele ya waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, aliyekuwa
Mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania iliyomaliza muda wake Hashim
Lundenga amesema kuwa kamati mpya ndiyo itakayowajibika na shughuli zote
zilizokuwa zikifanywa na kamati ya awali.
Amesema
kamati hiyo itafanya kazi zake kwa kuzingatia sheria na vigezo vyote
vya kimaadili ili kuepuka ukiukwaji wa taratibu za mashindano hayo.
“Hatutamvumilia
mwanakamati yeyote atakayevunja miiko ya mashindano haya, sisi tutakuwa
nyuma tukiangalia kwa umakini”, amesema Bw. Lundenga.
Kwa
upande wake Mwenyekiti mpya wa kamati hiyo Juma Pinto ametoa pongezi za
dhati kwa kamati iliyomaliza muda wake na kuhaidi kukubaliana na mfumo
unatumika kuratibu mashindano hayo .
“Namshukuru Lundenga kwa
kunikabidhi nafasi hii ya mwenyekiti wa kamati ya miss Tanzania, naahidi
kuratibu mashindano haya kwa kuzingatia vigezo na masharti yaliyowekwa
ili kamati yangu iweze kukidhi haja ya mashindano haya”. Amesema.
Naye
Msemaji Mkuu wa kamati hiyo na aliyekuwa Miss Tanzania namba mbili
mwaka 2006 Jokate Mwegelo, ametoa rai kwa wasichana wa kitanzania
wajitokeze kushiriki mashindano hayo kwa kuonesha vipaji walivyonavyo na
kupata ajira.
Mwishoni
mwa mwaka jana Mashindano ya Miss Tanzania yalikumbwa na mtafaruku wa
ukiukwaji wa maadili na vigezo vya mashindano na kulazimika kusimamishwa
kwa muda na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).
Kamati Mpya ya Miss Tanzania inaundwa na wajumbe wafuatao
1.Juma Pinto – Mwenyekiti
2.Lucas Rutta – Makamu Mwenyekiti
3.Doris Mollel – Katibu Mkuu
4.Jokate Mwegelo – Msemaji wa Kamati
5.Hoyce Temu – Mjumbe
6.Mohamed Bawazir – Mjumbe
7.Gladyz Shao – Mjumbe
8.Magdalena Munisi 0 Mjumbe
9.Shah Ramadhani – Mjumbe
10.Hamm Hashim – Mjumbe
11Khalfani Saleh – Mjumbe
12.Ojambi Masaburi – Mjumbe
Kwa upande wa Sekretariet tunao wajumbe 4 ambao ni
1.Dr.Ramesh Shah
2.Hidan Ricco
3.Yasson Mashaka
4.Deo Kapteni

No comments:
Post a Comment