Timu za TP Mazembe ya Congo DRC na Mamelodi Sundowns ya nchini Afrika
Kusini zinatarajiwa kuwasili Tanzania kwa ajili ya kucheza mashindano
maalumu ya kumuaga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete anayemaliza muda muda wake madarakani kama Rais mwezi
Octoba mwaka huu.
Klabu hizo zitaongozana na wamiliki wake ambapo Moise Katumbi
ataongozana na klabu yake ya TP Mazembe kwenye safari hiyo ya kuja
Tanzania wakati Patrice Motsepe nae atakuja pamoja na timu yake ya
Mamelodi Sundowns kuja kumuaga Rais Kikwete katika mashindano hayo
maalumu .
Kwa upande wa Tanzania, timu mbili zitakazothibitisha mapema ushiriki
wake kati ya Azaim FC, Yanga SC na Simba SC zitapata fursa ya kushiriki
mashindano hayo maalumu ya kumuaga Dkt. Jakaya Kikwete ambayo
yatashirikisha timu nne mbili zikiwa ni TP Mazembe na Mamelodi Sundowns
na timu mbili za Tanzania.
Rais Kikwete anafahamika kwa kuwa miongoni mwa marais wa Tanzania ambao
wanapenda michezo na amesaidia kwa kiasi kikubwa kukua na kuendelea kwa
michezo nchini husunan soka katika kipindi chote ambacho amekuwa
madarakani.
No comments:
Post a Comment