STAA wa filamu Bongo, Chuchu Hans.
STAA wa filamu Bongo,
Chuchu Hans ameamua kumfuata mchumba wake ambaye pia ni muigizaji,
Vincent Kigosi ‘Ray’ katika vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa).
Akizungumza na paparazi, Chuchu alisema kuwa kupitia Ukawa, ameamua kuingia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kuanzia sasa atambulike kama mmoja wa wanachama wa chama hicho.
“Nimeamua kumfuata mchumba
wangu Ray baada ya kujiona sina chama cha kwenda, na soon nitaanza
kuonekana katika magwanda,” alisema Chuchu.

No comments:
Post a Comment