19 June 2012

HATIMAYE WOLPER ANYANG'ANYWA GARI


 Mwigizaji ‘five star’ kutoka tasnia ya filamu Bongo, Jacqueline
Wolper Masawe, amenyang’anywa ‘mkoko’ (gari) wa kifahari
 aliokuwa akitanua nao katika mitaa ya mbalimbali ya jiji la Bongo.
Habari zenye ukweli 100% ambazo Teentz.com imezinyaka zinasomeka
 kuwa Wolper anayejulikana kama Amber Rose wa Bongo amenyang’anywa
mkoko huo aina ya BMW X6 wenye thamani ya ‘ngawira’ za kibongo ML 170,
 sambamba na kupigwa ‘stop’ kukaribiana na mshefa aliyekuwa amemnunulia
ndinga hiyo.
Kwa mujibu wa chanzo, hatua ya mshefa huyo kuamua kuchukua ndinga yake
 ni baada ya kugundua kuwa Wolper anatoka kimapenzi na ‘sharobaro’ mmoja
 anayemiliki duka maarufu la viwalo pande za Kinondoni.
Aidha chanzo hicho, kimeieleza Teentz.com kuwa hivi sasa mwanadada huyo
ameamua kutembelea ndinga aina ya Noah aliyokuwa akitembelea zamani.

Chanzo-Teentz.com

1 comment:

  1. vya bure vina madhara sana kuweni makini dadazangu,mtaaibika mjini hapa.

    ReplyDelete

Comments system

Disqus Shortname