Msaniii Nuhu Mziwanda ambaye kwa sasa anafanya poa na wimbo wake mpya
'Bilima' amefunguka na kusema kuwa kwa sasa hayupo na Shilole, Nuhu
amesema hayo leo alipokuwa Kikaangoni akichat na mashabiki kupitia
ukurasa wa facebook wa EATV.
Tweet
Toka ulipoaanza mwezi wa ramadhan kulikuwa na tetesi kuwa msanii Nuhu
amehama kutoka kwa Shilole na sasa anaishi kwake mwenywe hilo
limethibitishwa Nuhu alipokuwa akijibu swali la kwanini mpaka sasa
anaendelea kuishi na Shilole kwenye nyumba ambayo Shilole amepanga.
"Hapana sipo na Shilole kwa sasa mimi nipo kwangu"
Lakini kauli ya Nuhu haina maana kuwa mapenzi yao yamekufa lahasha bali
amempisha mwenzake katika kipindi cha mfungo wa ramadhan kutokana na
misingi ya imani ya mpenzi wake na kudai kuwa licha ya hilo hivi sasa
yeye mwenyewe anakwake na anamaisha yake mwenyewe.
Maswali mengi ambayo mashabiki wa ukurasa wa EATV walikuwa wakiyauliza
yalikuwa ni kuhusu maisha ya mapenzi kati yake na Shilole hivyo walikuwa
wakihitaji kufahamu mambo mbalimbali ambayo huenda wanaona kama
yanazushwa na jamii hivyo ilikuwa ni sehemu ya wao kupata ukweli,
mashabiki wengi walikuwa wakiiuliza inakuaje anakubali kupigwa pigwa na
mwanamke kama mtoto na hapo ndio Nuhu Mziwanda alipoweka wazi suala hilo
la yeye kupewa kichapo na Shilole.
"Hamna mapenz bila kugombana na siku zote ukitaka kudumu na mwanamke
usimuonyeshe ubabe sababu mwanaume wa kweli hapigi na hata kama ukipigwa
kibao na mwanamke hauwezi kufa hivyo ni vema kua kama mwanaume na
kusamehe"
Mbali ni hilo Hit maker huyo wa Bilima alikana suala la yeye kulelewa na
Shilole na kusema kuwa yeye ana maisha yake na mpenzi wake huyo ana
maisha yake pia hivyo halelewi kama ambavyo baadhi ya watu wanavyosema
mitaani kuwa analelewa na kutunzwa na Shilole.
"si kweli mimi silelewi maana nina maisha yangu na shishi ana maisha
yake so tumekutana tu kimapenzi ila watu wanajudge tofauti ila wanapaswa
kutambua kuwa mimi na maisha yangu na Shishi pia ana maisha yake
binafsi,ni mapenzi tu yanafanya kuwa kitu kimoja"
MATUMIZI YA LUGHA
Msanii huyo amekiri wazi kuwa yeye lugha ya kiingereza si lugha yake
hivyo makosa ambayo anakuwa anayafanya katika matumizi ya lugha hiyo ni
ya kawaida sababu tu si lugha yake ila anazidi kujifunza zaidi ili aje
kuwa na matokeo mazuri katika kutumia lugha hiyo ya kiingereza, hivyo
anakubali wazi kuwa kile alichokuwa amepost katika mitandao yake ya
jamii haikuwa makusudi bali ni bahati mbaya na yote ni sababu ya
kutofahamu lugha hiyo kwa undani zaidi
"kingereza si lugha yangu nilikosea kweli ila bahati mbaya ila nazidi
kujifunza, hivyo tegemeeni matokea mazuri kwenye hiyo lugha toka kwangu"
IMANI ZA KISHIRIKINA
Baadhi ya mashabiki wamekuwa wakisema kuwa msanii huyo anajihusisha na
imani za kishetani kwa kutumia alama ya 666 katika mitandoa yake ya
kijamii,lakini yeye amekuja kuweka wasa na kusema kuwa yeye anamuamini
Mungu hivyo hana imani hizo lakini pia amesisitiza kuwa haamini kama
namba hizo zinatumika na watu wanao amani ushetani,
"Sina imani hizo na siamini kama hiyo namba ni illuminat na kingine
ukiamini hiyo namba ni illuminat basi itakudhuru ila mimi na muamini
Mungu tu"
Katika safari yake ya Maisha Nuhu Mziwanda anasema hataweza kusahau
kamwe siku aliyosafiri na kwenda nje ya nchi halafu akaachwa kwenye
treni na wenyeji wake anadai hiyo siku katika maisha yake haitakuja
kusaulika kirahisi,na kwa kumalizia aliweza kuweka wazi kuwa anatarajia
kuja kufunga ndoa na Shilole na kuoana naye kama Mume na Mke kwa sababu
anamiini kuwa wanapenda na ndiyo maana bado wapo pamoja sasa kwa mwaka
wa pili katika mahusiano yake
No comments:
Post a Comment