Na Gideon Mwakanosya-Songea
JESHI la Polisi mkoani Ruvuma linamsaka mganga wa kienyeji ambaye jina lake limehifadhiwa mkazi wa eneo la Lilambo manispaa ya songea kwa tuhuma za kumnywesha dawa Lucia Zimbili (65) mkazi wa kijiji cha Maposeni Peramiho ambaye inadaiwa alikuwa analalamikiwa na ndugu zake kuwa amemroga Edward Soko aliyefariki dunia siku chache kabla ya tukio hilo.
Habari zilizopatikana jana ambazo zimezibitishwa na kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela zimesema kuwa tukio hilo limetokea Julai 12 mwaka huu majira ya saa za usiku huko katika eneo la Lilambo nje kidogo ya manispaa ya songea.
No comments:
Post a Comment