09 July 2015

Mwandosya awaangukia UKAWA

KUTOKANA na wabunge wanaounda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA), kutangaza kutomsikiliza Rais, Jakaya Kikwete wakati wa hotuba yake ya kuvunja bunge, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Profesa Mark Mwandosya, ameibuka na kutaka bunge litunge kanuni zinazowataka wabunge wote kuwapo bungeni wakati rais anapokuwa akilihutubia Bunge
Amesema iwapo itatungwa kanuni hiyo itawalazimisha baadhi ya wabunge wenye tabia ya kususia vikao vya Bunge katika mazingira yasiyokubalika. Kauli ya Prof .Mwandosya ilionesha moja kwa moja kuwalenga wabunge wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ambao wamesusia vikao vya Bunge mwanzoni mwa wiki hii japo hakuwataja.
Kwa pamoja wabunge hao wakiongozwa na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, walichukua uamuzi huo baada ya kutoridhishwa na hatua ya Serikali ya kuwasilisha na kupitisha miswada ya sheria ya mwaka huu inayohusu masuala ya gesi, mafuta na petroli.
Amesema kitendo cha kuodoka bungeni wakati rais wa nchi anatarajia kulihutubia Bunge ni tukio la fedheha na halitakiwi kuungwa mkono.
Amesema duniani kote ujio wa rais katika Bunge ni jambo muhimu kitaifa.
Alieleza kwamba bora itungwe kanuni ya kuwalazimisha wabunge wote kuwapo bungeni siku rais anapokwenda bungeni vinginevyo mbunge awe na sababu maalum.
Wakati Mwandosya akisema hayo, Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (UDP), naye alionyesha kutoridhishwa na tabia ya wabunge wa Ukawa kususa vikao vya Bunge

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname