14 July 2015

EDWARD LOWASSA BAADA YA LUKATWA HAYA NDIO YANAYOMSUMBUA MPAKA KUKOSA RAHA

Nimepata taarifa kutoka kwa watu walio karibu na Lowasa kuwa tangu juzi chakula hakijapanda kwa mzee. Kwamba kila akiwekewa chakula mezani, anachokonoa kidogo tu na inachukua muda mrefu kati ya tonge moja hadi jingine. Pia mdau huyo kanidokeza kuwa Mzee Lowasa kwa sasa ana mawazo mengi sana na hajui afanye nini. Wapo waliomshauri kuwa akae kimya katika kipindi hiki kigumu ili apate muda wa kutosha kutafakari na kufanya maamuzi. Hata hivyo, ushauri huo ameutupa kwani anahisi kwamba muda ukipita
atasahaulika na yale aliyopanga kuyatekeleza hayatatimia. Wapo waliomshauri kwamba aende kwao Monduli akatulie japo kwa wimbi mbili na asiruhusu watu wamtembelee ili mawazo yake yapungue. Wapo pia wanaomshauri kuwa aende kwenye vyombo vya habari na kueleza kwa nini amekatwa. Wanaomshauri hivyo wanaona kuwa hiyo ndo njia sahihi kwani kukaa kwake kimya kunaacha sintofahamu kwa wapenzi wake. 

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname