AY amefungua njia ya mafanikio kwa wasanii wengi wa Tanzania. Miongoni mwa watu walionufaika na mashavu yake ni Diamond.
Katika ujumbe wake wa kumpongeza AY kwenye siku yake ya kuzaliwa
Jumapili hii, Diamond amedai kuwa AY ndiye aliyemuunganisha na Davido
hadi wakafanya remix ya wimbo wake ‘Number One’ uliobadilisha maisha
yake.
“Misingi na Daraja Imara la kimataifa ulio tujengea na unayozidi
kutujengea ndio leo inatusaidia vijana wako nasi kuweza kupenyeza na
kutangaza kazi zetu kimataifa,” ameandika Diamond kwenye Instagram.
“Pengine watu hawajui kuwa wewe ndio uliyeniwezeshea kufanikisha
Collabo langu na Davido, Kuniunga na Godfather na vingi ambavyo naamini
ndio Mwanzo wa safari yangu ya Kimataifa… Nakuheshim sana Brother, na
daima nitahakikisha sikuangushiemoji…Happy birthday Bro.”
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, AY ameandika:
July 5, 1982 Ambwene Yessayah alizaliwa. Namshukuru Mungu kwa
kuiona siku hii ya leo. Nawashukuru wazazi wangu kwa kunileta duniani.
Mungu awalaze mahali pema peponi. Natamani mama yangu angekuwa hai aone
jinsi kijana wake alivyokuwa mkubwa na pengine afurahie jasho lake la
kunizaa, kunilea na kunitunza.
Nawashukuru wote walio na mchango mkubwa kwenye maisha
yangu, ni wengi siwezi kuwamaliza kuwataja. Navikushukuru vyombo vya
habari vyote kwa support kubwa inayoendelea kunipa. Nakushukuru pia wewe
shabiki yangu kwa kuendelea kuniunga mkono. Thank You!!
No comments:
Post a Comment