08 July 2015

ALI KIBA NAE AFUNGUKA LIVE: ASEMA HANA BIFU NA DIAMOND PLATINUMS


Get a life guys, Diamond na Alikiba hawana beef yoyote… at least kutoka kwa kauli zao wenyewe.
Superstars hawa wa Tanzania weekend na wiki hii walikuwa na interview kwenye vyombo tofauti vya habari na kuulizwa swali linalofanana,” mna beef?”
“Beef hakuna, mimi sidhani kama kuna hiyo kitu,” Alikiba aliambia One on One ya Citizen TV Ijumaa iliyopita.


“Sisi ni wasanii kuna watu wanatuangalia, then tuko na fans, Diamond ana fans wake, mimi nipo na fans wangu. Sometimes they do it for fun you know that’s what I know from my opinion. Mimi na Diamond hatujawahi kukutana sehemu tukagombana tukasemeana hivi,” alisema Kiba.
“Vile vile kitu ambacho sipendi ni mimi kufananishwa na Diamond. Mimi nafanya muziki wangu ambapo hakuna mtu anaweza kufanya muziki wangu sababu kila mtu ana talent yake and I believe I am versatile, nin hicho kipaji cha kubadilika kila wakati. So kama Diamond yuko interested kufanya featuring na watu wengine mimi nafanya muziki ninaotaka mimi na yeye anafanya wa kwake kila mtu ana style yake ya ufanyaji muziki,” aliongeza.  


BOFYA KUSOMA KAULI YA KIBA

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname