08 July 2015

WEMA SEPETU! AGUNDULIKA NA GONJWA LA AJABU! MWENYEWE AFUNGUKA HAYA...

Staa wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu. Gonjwa hilo limegundulika hivi karibuni machoni mwa paparazi wetu baada ya kumuona mlimbwende huyo wa Tanzania mwaka 2006 akiwa na bonge la nundu nyuma ya shingo, jambo lililomfanya paparazi ashindwe kujizuia na kuamua kumuuliza Wema.
Habari mbaya ikufikie kuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Endless Fame Films Productions ambaye yupo kwenye harakati za kuwania Ubunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Singida, Wema Isaac Sepetu amegundulika kuwa na gonjwa la ajabu linalomsababishia kukosa raha ambalo linakua kadiri siku zinavyosonga.

Bila kupepesa macho Wema alisema kuwa ‘uvimbe’ huo upo mwilini mwake kwa zaidi ya miaka 26 sasa na umekuwa ukiongezeka siku hadi siku.
Wema alilazimika kufunguka zaidi baada ya paparazi wetu kumuona sehemu hiyo ikiwa imemvimba bila kujua kama ni tatizo lake la miaka yote.


No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname