11 June 2015

Rais Kikwete azuiliwa kuingia Denmark

Rais Wa Tanzania ndugu Jakaya Mrisho Kikwete amezuiliwa kuingia Denmark kutokana na vuguvugu la uchaguzi nchini humo baada ya kubainika kuwepo kwake kungempa nafasi zaidi ya kuonekana waziri mkuu Wa sasa kitendo kilichotafsirika Kama kumpigia kampeni.


RAIS Jakaya Kikwete ambaye amekuwa katika ziara za kuaga washirika wa mandeleo katika nchi za Scandinavia, amekataliwa kuingia Denmark kwa madai kuwa ziara yake itatumika kisiasa kumnufaisha Waziri Mkuu wa sasa wa Denmark.

Nchi hiyo inatarajia kufanya uchaguzi wake mkuu wiki ijayo. Zuio hilo limekuja baada ya vyombo vya habari na vyama vya siasa kudai kuwa ziara hiyo ingetumika kumnufaisha Waziri Mkuu aliyepo kwa kumpa muda wa ziada mbele ya vyombo hivyo wakati huu wa kampeniVyama vyote vya kisiasa vinapata muda sawa mbele ya vyombo vya habari na kwa hiyo uwepo wa Rais Kikwete nchini Denmark ungesababsha Waziri Mkuu aliyepo madarani kuonekana mara nyingi akimpokea mgeni wake.

Rais Kikwete hivi karibuni amefanya ziara katika nchi za Finland, Sweden, Uholanzi ikiwa ni sehemu ya kuaga kutokana na muda wake wa kuwa madarakani kufikia ukingoni.


MY TAKE:
Vyombo vya habari hapa kwetu vijifunze kutoka kwa Wenzetu viache ushabiki na viweke mizani sawa kwa wagombea na vyama vyote.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname