Mwanasiasa mkongwe wa CCM mzee John Malecela amemshangaa mzee kingunge na kumuita Yuda na msaliti, ndumilakuwili na mchochezi na hana shukurani hakumbuki alichofanyiwa na serikali ya Kikwete huyu Kingunge.
Anakusanya ushuru stendi ya Ubungo na maeneo mengine ya mji hela anazokusanya kila siku anampa nani au aliwashawahi kutoa msaada wowote kwenye kituo cha kulea watoto yatima? Mzee Malecela amesema kingunge aache kabisa kuwachagulia mtu anayefaa kuwa Rais kazi hiyo ipo mikononi mwa CCM kwenye mkutano mkuu hata CHADEMA, CUF hufanya hivyo kwenye vikao vyao maalumu.
Mzee Malecela amesema kura ya veto iliyomtoa manyoya yeye wakati anagombea Urais ndio itakayotumika kuangalia mgombea mwenye Sifa zote zinazohitajika kwa Tanzania ya sasa na nyingine pia awe msafi, mpole, mchana Mungu mwenye maadili. Mzee amesema Rais hawezi kupatikana kwa kelele za watu, polojo na maigizo muda ukifika kila Mgombea atabeba msalaba wake.
Kwa matendo waliyoyafanya kugawa watu kwa kuwanunua kwa uchu wa madaraka, mbegu hiyo ni mbaya sana kwa Taifa kwani kuna uwezekano Taifa lilitagawanyika tusipokuwa makini na wasaka urais kwa nguvu.
No comments:
Post a Comment