Hali hiyo inawaweka kwenye position ya kuwajua in and out wanasiasa wote hususan wale wanaotarajia kugombea nafasi za juu hasa ya Urais.
Mwandosya anasema kuwa kitendo cha Wakuu hao baada ya kustahafu kujihusisha na siasa kwa kuamua kugombea nafasi za kisiasa au kuwaunga mkono baadhi ya wanasiasa wanaogombea nafasi za kisiasa kunawaweka kwenye nafasi ya kukiuka maadili ya kazi zao. Anasema kuwa ijapokuwa wanapostahafu wanaacha mafaili ofisini, wanaondoka na kumbukumbu moyoniPia anasema kuwa wakuu hao bado wanakuwa na mahusiano na watumishi waliopo hivyo inakuwa ni jambo jepesi kwao kujijenga au kumjenga mtu wanayemuunga mkono kupitia watumishi wa vyombo hivyo wenye mahusiano mema nao.Pia anasema kuwa wakuu hao wanaweza kumbomoa adui wao kirahisi kwa kwa sababu hizo hizo.
Ijapokuwa Prof Mwandosya hakutaja moja kwa moja majina ya anaowalenga, lakini kwa mtiririko wa matukio ya hivi karibuni, anamlenga Apson Mwang’onda. Kwa nini nimefikia hitimisho hilo? Kwa siku kadhaa nimekuwa imekuwaikiripotiwa habari zinazomhusu Apson Mwang’onda akijihusisha na Mtandao wa Lowasa.
Kwamba, Apson Mwang’onda ni Mwenyekiti wa Kamati ya Wezesha Lowasa aende Ikulu na kwamba amekuwa akifanya vikao na wanasiasa kadhaa wanaomuunga mkono Lowasa. Vikao hivyo vimekuwa vikifanyika nyumbani kwa Apson na Mtoto wake Jimmy ambavyo pia vimekuwa vikihusisha matumizi ya kiasi kikubwa cha fedha. Apson Mwang’onda amesikika akisema kuwa yeye kwa sasa ni mstahafu hivyo si tatizo kwake kujihusisha na siasa.
Katika Kitabu alichoandika kijulikanacho Sauti ya Umma ni Sauti ya Demokrasia, Prof Mwandosya ameeleza jinsi alivyohujumiwa na baadhi ya watendaji wa serikali na chama na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa, Apson Mwang’onda. Katika kitabu hicho, Profesa Mwandosya ametaja mlolongo wa viongozi na watendaji wa serikali katika kitabu hicho, miongoni mwa majina hayo limo la Apson.
Katika kitabu hicho Profesa Mwandosya anasema kuwa alipekewa ujumbe na mzee Jimmy David Ngonya kwamba amekuwa anamlaumu Apson kumhujumu katika harakati za kuwania nafasi ya NEC kwa mkoa wa Mbeya mwaka 2007. Katika kinyang’anyiro cha nafasi ya NEC mkoa wa Mbeya Profesa Mwandosya alipambana na Thom Apson Mwang’onda. Katika kitabu hicho Profesa Mwandosya, anaelezea jinsi alivyofanyiwa fitna, hujuma na kila aina ya mizengwe wakati wa mchakato wa uchaguzi kwa mwaka 2007 mkoani Mbeya.
Katika ukurasa wa 21, ameelezea baada ya Chimwaga, siku moja aliyekuwa naye karibu sana Mwalimu Jimmy David Ngonya alimtembelea nyumbani kwake Kibisi Tukuyu mwaka 2006, na kumpa ujumbe wa Apson ambao alimpa baada ya kufanya naye mazungumzo katika hoteli ya Land Mark iliyopo mjini Tukuyu.
Katika kitabu hicho pia ukurasa wa 141 wa Profesa Mwandosya anaeleza taarifa alizopata za matumizi makubwa ya fedha katika uchaguzi wa nafasi ya NEC mkoa wa Mbeya.
“Makadirio ya fedha walizotumia yalikuwa kati ya Sh. milioni 300 hadi bilioni moja,” anaeleza Profesa Mwandosya kwenye kitabu hicho wakati akielezea mchuano ulivyokuwa katika kinyang’amyiro cha ujumbe wa NEC mkoa wa Mbeya. Anasema kuwa katika mazingira ya matumizi makubwa ya fedha ulikuwa ni ushindani kati ya ‘Goliati’ mwenye fedha na ‘Daudi’ asiye na fedha.
No comments:
Post a Comment