Mshiriki wa Big Brother Afrika ‘BBA’
Hot Shot 2014 kutoka nchini Namibia, Luis Munana, amemwagia sifa
aliyekuwa Miss Tanzania 2016, Wema Sepetu kuwa ni mwenye mvuto wa
kipekee.
Lakini licha ya kutoa sifa hizo, mshiriki mwenzao ambaye
ndiye mwenyeji wao, Idris Sultan, hakutokea katika sherehe hiyo jambo
lililozua minong’ono kwa watu baada ya tetesi kwamba ana ugomvi na Wema
Sepetu.
Wema alimwagiwa sifa hizo alipokuwa katika sherehe za Instagram Party katika viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
“Wasanii
ninaowakubali kutoka Tanzania ni Wema Sepetu, ni mrembo sana nampenda,
wasanii wengine ambao nawakubali ni Shilole, Ommy Dimpoz pamoja na wimbo
wake wa Wanjera,” alisema.
Washiriki wengine wa BBA waliohudhuria sherehe hizo ni Nhalanhla na Samantha wote kutoka nchini Afrika Kusini.
Wasanii
wa Tanzania waliohudhuria sherehe hiyo ni Ben Paul, Izzo Bizness,
Shelta, King Majuto, Stan Bakora, JJ Band, huku mshereheshaji akiwa Adam
Mchomvu, B Dozen na DJ Ommy.
Hata hivyo, Wema alishukuru kupendwa na
Luis. “Jamanii sina hata la kusema jinsi ulivyonisifia, nashukuru sana
sana,” alijinadi Wema akishukuru.
No comments:
Post a Comment