Staa
wa sinema za Kibongo, Haji Adam ‘Baba Haji’ akivishwa pete na mkewe
Latifa Sharji. Kabla ya pati hiyo iliyochukua nafasi kwenye Ukumbi wa
Escape One uliopo Mikocheni, Dar usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita,
Baba Haji alifunga ndoa na Latifa katika Msikiti wa Bungoni, Ilala
jijini Dar.
SAA chache kabla ya kuanza kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani,
staa wa sinema za Kibongo, Haji Adam ‘Baba Haji’ ameangusha bonge la
harusi baada kufunga ndoa na mrembo aliyetajwa kwa jina la Latifa Sharji
wiki moja iliyopita huku mastaa wakifanya kufuru kama kawaida yao.
Katika
pati hiyo iliyohudhuriwa na mastaa kibao wa Bongo Movies huku gazeti
hili nalo likijipenyeza ndani, waalikwa walikula na kunywa hadi wakasaza
kabla ya muda wa zawadi na kusakata muziki.Kwenye shughuli hiyo, kadiri
watu walivyokuwa wakipiga ulabu ndivyo sherehe ilivyokuwa ikichangamka
na mastaa kujikuta wakiserebuka muziki kwa kwenda mbele.
Jacqueline
Wolper Massawe, akisakata rhumba. Muda wa kutunza ulipowadia ndipo
mastaa walipoanza kushindana kuwamwagia wanandoa hao ‘minoti ya wekundu
wa msimbazi’.
Baadhi ya wasanii walioongoza kutunza ni tajiri mfupi,
Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ambaye alimwaga fedha taslimu Sh.
milioni 2 akifuatiwa na Single Mtambalike ‘Richie’, Jacob Steven ‘JB’,
Vincent Kigosi ‘Ray’ na wengine waliokuwa fedha za kudunduliza.
Kwa
upande wa mastaa wa kike, Kajala Masanja ‘Kay’ aliongoza kwa kumwaga
mkwanja akifuatiwa na Jacqueline Wolper Massawe, Wastara Juma, Jennifer
Kyaka ‘Odama’, Lulu Mathias Semagongo ‘Anti Lulu’ na watoto wengine wa
mjini.
Muda
wa kuserebuka ulipofika ilikuwa ni balaa tupu kwani Wolper aliweka
shida chini, akatupa mikono kule na kumwaga mauno hadi akajikuta
akimwaga ‘lazi’.
Hadi gazeti hili linaanua jamvi ukumbini hapo usiku
mnene, baadhi ya mastaa walikuwa wakiendelea kusakata rhumba na kupiga
kinywaji
No comments:
Post a Comment