05 June 2015

MAKAVU LIVE: OMMY DIMPOZ, MARTIN KADINDA NDO’ MAMBO GANI HAYA SASA?!

OMARY Faraji Nyembo, anayefahamika zaidi kimuziki kama Ommy Dimpoz ni msanii mwenye jina kubwa katika fani, ingawa ni miongoni mwa vijana waliochipukia na kupata umaarufu katika miaka ya hivi karibuni. 
Amefanya kazi nyingi nzuri na zilizopata kupigwa sana katika vituo vingi vya redio na televisheni, baadhi yake vikiwa ni pamoja na Baadae, Me and You, Ndagushima na Wanjera, kitu kinachomfanya kuwa miongoni mwa wasanii wanaofanya vizuri katika soko la Bongo Fleva kwa sasa. 
Ingawa hatambi sana, lakini uwezo na kazi zake kwa sasa unamfanya kuwa mmoja wa wasanii ambao kukosekana kwake katika shughuli yoyote kubwa ya burudani ni kero kwa mashabiki. Anategemewa kuwepo miongoni mwa vijana kumi bora wa muziki wa kizazi kipya. 
Kwa upande wake, Martin Kadinda ni miongoni mwa wabunifu vijana wa mavazi hapa nchini, ingawa fani hii haimpi jina sana kama ile ya kuwa meneja wa muigizaji Wema Sepetu. Lakini kiukweli, Martin yupo sana kwenye ubunifu na mitindo.
Nimemfahamu kitambo kidogo, akishiriki kupanda jukwaani kusindikiza nguo zilizobuniwa naye au ‘dada zake’ Khadija Mwanamboka na Asia Idarous au wabunifu wenzake akina Ally Rhemtulah. .  


No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname