Gladness Mallya na Hamida Hassan
MAKUBWA!
Yule bwana ambaye ni kigogo serikalini (jina tunalihifadhi kwa sasa)
aliyekuwa na uhusiano wa kimapenzi na staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu
na kumwagana naye, taarifa zimevuja kwamba kwa sasa amemnasa mwigizaji
Ester Kiama ambaye anampa jeuri ya kuishi mjini.
Kwa mujibu wa
chanzo makini, kigogo huyo ambaye anamiliki maduka kadhaa ndani ya
Mlimani City, ndiye anayempa jeuri Ester kwa kumfungulia biashara
mbalimbali na fedha kwa ajili ya kutengeneza filamu zake mwenyewe licha
ya kuwa mrembo huyo naye ana biashara zake nyingine ikiwemo ya kuuza
magari.
No comments:
Post a Comment