Wachezaji na makocha wa Mwadui FC
wamenusurika kifo baada ya gari walilokuwa makiendesha kuelekea
Shinyanga kupata ajali na kupinduka mara tano kabla ya kusimama.
Wachezaji walionusurika kwenye ajali hiyo ni golikipa Shabani Kado pamoja na kiungo Nizar Khalfan.
Wachezaji hao wakiwa na makocha
Habib Kondo na Khalid ( kocha wa makipa) walikuwa njiani kwenda kujiunga
na kambi ya timu yao ya Mwadui FC.
“Sababu ya gari kupinduka ilikuwa
ni baada ya tairi la nyuma kuchomoka,baada ya hapo gari ilipinduka
karibia mara tano,hatukuumia sana isipokuwa mimi tu nilipata michubuko
kwenye mkono”, Shabani Kado ameuambia mtandao huu
No comments:
Post a Comment