Mama Eugene Mwaiposa enzi za uhai wake
Naibu
Spika ndg John Ndugai ameliahirisha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Kufuatia Kifo cha aliyekuwa Mbunge wa UKONGO Kupitia chama Cha
Mapinduzi (CCM) mh. Eugene Mwaiposa aliyekutwa amefariki nyumbani kwake
Mapema leo Asubuhi, Tangazo hilo la Naibu Spika Bungeni limeeleza chanzo
cha Kifo hicho kuwa ni Shinikizo la Damu.
TAARIFA YA NAIBU SPIKA
Bunge
la jamhuri limepata msiba wa kufiwa na mbunge wa jimbo la Ukonga,
alikuwa na tatizo la shinikizo la damu kwa muda mrefu, Amefariki
nyumbani kwake hapa Dodoma. Nyumbani kwa marehemu ni eneo la Chaduru
opposite na jengo jipya la hoteli ya Shabiby barabara ya Dar es Salaam,
Mwili umepelekwa hospitali ya mkoa wa Dodoma kwa uchunguzi zaidi.
Shughuli
ya Kuaga itafanyika kesho baada ya familia yake kuwasili hapa Dodoma.
Tutatumia mtandao wa simu kuwajulisha taarifa zaidi, kwa jinsi hio
natumia kanuni ya 152 kuahirisha bunge hadi keshokutwa Alhamis.
No comments:
Post a Comment