Polisi
kutoka Mji wa Atlanta waperipoti kumkamata mtu aliyejaribu kumuua Mkali
wa Hipohop Lil Wayne kwa kupiga risasi basi lake la safari.
Kwa mujibu wa ripoti ya
Polisi wamemtaja mtu huyo anayejulikana kwa jina la Jimmy Carlton
Winfrey na ni mtu wa karubu wa Young Thug.
Kwa Mujibu wa maelezo
aliyoyatoa kwenye kituo cha polisi baada ya kufanyiwa mahojiano, Jimmy
Carlton Winfrey alisema aliamua kupiga basi hilo ili pate heshima ndani
ya kundi lake la Bloods Gang.
Bado hukumu yoyote
haijatolewa na polisi wamesema wanaendelea na uchunguzi ambapo kesi hiyo
itapandishwa mahakani kwa ajili ya kutoa hukumu.
Wiki kadhaa zilizopita
iliripotiwa kupigwa risasi basi la Lil Wayne lillokuwa likipita kwenye
mji wa Atlanta huko Marekani, mji ambao anaishi hasimu wake mkubwa kwa
sasa Young Thug.
No comments:
Post a Comment