02 June 2015

Bifu la Emelda Mwamanga wa Bang magazine na Reginald Mengi Kwa Kuvujisha Picha za Mengi na Familia yake


Mwanamama mjasiriamali, na managing director wa jarida maarufu nchini , Bang magazine , aitwaye Emelda Mwamanga amefunguka kuhusu bifu lake na mfanyabiashara maarufu nchini, Reginald Mengi, kupitia kwenye moja ya mahojiano ya kwenye kipindi maarufu cha Tv Hapa nchini .

Mbali na kuelezea experience yake kwenye biashara yake, pia alizungumzia changamoto mbali mbali anazokabiliana nazo kwenye biashara zake, moja ya changamoto alizozielezea ni ile ya kushtakiwa na mfanyabiashara maarufu nchini, Reginald Mengi, ambaye ni mume wa aliyekuwa miss Tanzania, Jackline Ntuyabaliwe maarufu kama K-Lyn.

Akielezea chanzo cha kushtakiwa, mwenyewe anadai ni kuvujishwa kwa picha za mfanyabiashara huyo akiwa na familia yake, kitendo ambacho mfanyabiashara huyo hakukipenda hivyo aliamua kumshtaki mwanamama huyo kama adhabu na fundisho.

Akielezea kwa masikitiko mwanamama huyo alielezea jinsi ya picha hizo zilivyosambaa mitandaoni, ambazo zilipigwa mahsusi kwa ajili ya kupambwa kwenye jarida maarufu la mwanamama huyo, hata hivyo inasemekana baadhi ya wahariri wa jarida hilo walizivujisha picha za Mengi huyo kwenye mitandao ya kijamii either kwa bahati mbaya au kwa kukusudia , kitendo kilichomkera Mengi na kuamua kumshtaki.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname