22 June 2015

ALI KIBA ATANGAZA VITA NA DIAMOND! AFUNGUKA MAZITO! A-Z IPO HAPA MDAU...


Staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba. 

VITA! Saa chache tu baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar akitokea nchini Marekani kwa shughuli za kimuziki, staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ametangaza kile kinachotafsirika kuwa ni vita dhidi ya hasimu wake kwenye anga la muziki huo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Ijumaa Wikienda lina ‘full’ stori.
Ali Kiba alitema cheche Alhamisi ya wiki iliyopita ndani ya Hoteli ya Sea Cliff, Masaki jijini Dar, kulikokuwa na uzinduzi wa kampeni ya kupinga vita ujangili, iliyoratibiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, huku akiwa ni mmoja wa mabalozi sanjari na mlimbwende wa zamani, Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi ‘K-Lyin’.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz.   


No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname