Matumaini ya Taifa Stars kushiriki michuano
ya Chan yametoweka baada ya kupoteza mchezo wake wa kwanza nyumbani kwa
kufungwa na Uganda kwa mabao 3-0.
Stars imepoteza mchezo huo leo kwenye Uwanja
wa Amaan mjini Zanzibar baada ya kuchapwa na wageni wake Uganda.
Wakati leo imepoteza, inasubiri kusafiri
kwenda Uganda kuwavaa The Cranes, jambo ambalo linasubiri miujiza au aibu
zaidi.
Wakati Stars imepoteza mechi hiyo, Kocha
wake mkuu, Mart Nooij alitoka uwanjani hapo kama kiongozi wa serikali baada ya
kusindikizwa na askari pamoja na mtu mmoja mwenye umbo kubwa anayeaminika ni
mfanyakazi wa TFF.
Nooij amekuwa akipigiwa kelele na Watanzania
ambao wanaonekana wamechoka na kufungwa kila kukicha.
Mholanzi huyo anaonekana wazi kuishindwa
kazi yake, lakini TFF imekuwa inasita kumuondoa.
Hata hivyo, Watanzania wamekuwa wakipiga
kelele kuhusiana na Mshauri wa Ufundi wa Rais wa TFF aitwaye Peregrinus
Rutayuga ambaye anaonekana pia kuwa tatizo.
Wadau wamekuwa wakipiga kelele, Nooij, Rutayuga na memba wengine wa benchi hilo watupiwe virago.
No comments:
Post a Comment