11 May 2015

NISHA WA BONGO MOVIE AVAMIWA NA KUPOLWA MALI!!,SHUHUDIA GARI LAKE LILIVYO FANYWA

Gari la Nisha likiwa limeibiwa baadhi ya vitu.
STAA wa filamu za Kibongo, Salma Jabu 'Nisha' usiku wa kuamkia leo amevamiwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wapatao watano nyumbani kwake Kijitonyama jijini Dar na kuporwa baadhi ya mali.
Staa wa sinema za Kibongo, Salma Jabu 'Nisha'.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Nisha ameandika kuwa majambazi wapatao watano wakiwa na gari walivamia nyumbani kwake na kumpora huku akimshukuru Mungu maana yeye yuko salama.
Staa huyo pia aliweka picha ya gari lake lililokuwa limeibiwa baadhi ya vitu na majambazi hao kisha kuandika hivi:
Tukio hili limetokea ikiwa ni siku chache baada ya staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘Ali Kiba’ naye kuvamiwa na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi wapatao 20 nyumbani kwake Kunduchi, Dar kisha kumpora mali. TEMBELEA BLOG YETU KWA HABARI Z

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname