Floyd Mayweather akiwa kwenye bethidei ya Chris Brown.
NEW YORK, Marekani
NI
jeuri ya mkwanja! Ndivyo bondia Floyd Mayweather alivyoanza makeke ya
kutumia mkwanja wake baada ya hivi karibuni kufanya balaa la maana
kwenye siku ya kuzaliwa ya mwimbaji, Chris Brown.
Chris Brown akifungua 'shampeni'.
Hili
ni tukio la kwanza kufanywa na bondia huyo baada ya kutoka kumshushia
kichapo mpinzani wake, Manny Pacquiao, Jumapili iliyopita kwenye Ukumbi
wa MGM Grand Arena na kuweka historia ya kuwa bondia aliyepigana
mapambano yote bila kupoteza.
Mayweather,
ambaye aliambatana na mpenzi wake, Shantel Jackson na watu wake
wanaounda Kundi la Money Team, walikwenda kujumuika pamoja na Brown
katika siku yake hiyo ya kuzaliwa iliyofanyika kwenye klabu ya usiku ya
Las Vegas 'Super-club Drai's, ambayo ipo ndani ya Hoteli ya Cromwell.
Mayweather akiwa na totoz.
No comments:
Post a Comment