Staa
mrembo wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel ‘Mama Kijacho’ amesema baadhi ya
wasanii wa bongo movies hawajitambui ndio maana kazi zao nyingi hazina
mvuto badala yake nguvu nyingi wameelekeza kubuni skendo wakitarajia
ndio zitawatoa kisanaa.Alisema wasanii wengi wanatumia muda mwingi
kutafakari jinsi ya kutengeneza skendo ili watume kwenye mitandao na
kuandikwa kwenye magazeti lakini hawana ubunifu wa kutengeneza filamu
zenye ushawishi kwenye jamii.Aunt ambae kwenye filamu ya Chozi la Wanjaa
amecheza kama mke wa Dude alisema kwamba endapo wasanii wanaofanya mchezo huo hawata badilika ni ukweli usiopingika kwamba soko la filamu inchni litaendelea kudumaa kama ilivyo sasa.
amecheza kama mke wa Dude alisema kwamba endapo wasanii wanaofanya mchezo huo hawata badilika ni ukweli usiopingika kwamba soko la filamu inchni litaendelea kudumaa kama ilivyo sasa.
“Ni ukweli
kwamba baadhi ya wasanii wa filamu hawajitambui kwani akili yao
wameelekeza kwenye kutengeneza skendo badala ya kubuni namna ya kuigiza
filamu ambazo zinaweza kuwa na mvuto kwenye jamiiinayoziangalia kinyume
na hapo tutaendelea kusaka wachawi wanaoua soko letu’- Aunt Ezekiel
alilieza gazeti la Filamu
Mdau una maoni gani juu ya hoja hii ya wasanii kutengeneza skendo, je ni kweli? Msanii gani unahisi ndio kazi yake.
No comments:
Post a Comment