19 March 2015

PENNY SIJAWAHI BEBA MIMBA YA DIAMOND PLATINUMZ!

Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
IMEVUJA! Ile mimba ya aliyekuwa Mtangazaji wa Efm Radio, Penieli Mungilwa ‘Penny’ ambayo ilijulikana alipachikwa na staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ imezua mzozo upya baada ya kuvuja kwa madai mengine. Chanzo makini kimeliambia Amani kwamba, tofauti na madai ya Diamond kwamba Penny alitoa mimba yake, lakini kumbe Diamond hakumpa mimba ila ilikuwa ni magumashi ya Penny.
“Hali ilikuwa hivi! Kutokana na Diamond kutafuta mtoto kwa muda mrefu, hasa kwa mpenzi wake wa nyuma Wema Sepetu kushindikana, ikabidi Penny atumie mbinu yake ili kufaidika na pesa za Diamond.
“Penny aliahidiwa na Diamond kwamba, kama atakubali kuzaa naye atamnunulia gari zuri, kwa hiyo kazi ikawa kwa Penny sasa, afanyaje?
“Siku moja Penny alimwambia Diamond kwamba amenasa, Diamond akafurahi sana, lakini kumbe Penny alishaenda kwenye hospitali moja kubwa iliyopo Kinondoni (jina tunalo), akaongea na nesi mmoja kwamba kama atakwenda na Diamond kupima mimba akubali kwamba anayo, lengo lake ni kupata gari,” kilisema chanzo hicho.SOMA ZAIDI>>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname