20 March 2015

NYADHIFA MBALIMBALI ALIZOWAHI KUSHIKA MH.LOWASSA

Kikazi Lowassa amekulia na kufanya kazi zaidi katika serikali yake na chama hivyo ni mwanasiasa mkongwe mwenye uzoefu mbalimbali katika siasa za nchini Tanzania.Mara baada ya kumaliza chuo kikuu cha Dar es salaam aliajiriwa na CCM kama katibu msaidizi na baadaye Katibu wa Wilaya.
Alipata kuwa msaidiza wa mzee Rashidi Mfaume Kawawa, John Malecela, Daudi Mwakawago na Horace Kolimba. Alifanya kazi pia jeshini sambamba na Mh. Rais Jakaya Kikwete pamoja na Abdulrahaman Kinana na aliondoka jeshini akiwa na cheo cha Luteni.

Jambo moja ambalo watu wengi hatukulijua kabla ni kwamba Ndugu Lowassa ni miongoni mwa wanasiasa wanajeshi waliopigania vita nchini Uganda 1978/1979.
Kwa nchi nyingi duniani,hii ni sifa muhimu ya ziada kwa mtu yoyote anewania uongozi wa nchi kwa sababu kushiriki kupigana vita huchukuliwa kuwa ni kiwango cha juu kabisa cha uzalendo kwa kuwa tayari kuifia nchi yako.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname