Kila siku wauzaji wa dawa za kulevya
wamekuwa wakibuni njia mpya ya kusafirisha dawa hizo kwa nchi ambazo
zimepiga marufuku usafirishaji na utumiaji wa dawa hizo.
Mwanamke mmoja Uingereza amekamatwa baada ya kukutwa akiwa amebeba dawa za kulevya aina ya Cocaine ndani ya sidiria.

Mwanamke huyo
Nola Williams alikamatwa katika uwanja wa ndege wa
Gatwick, akitokea Jamaica akiwa na mtoto mdogo pamoja na kijana anaejihusisha na biashara hiyo ambaye jina lake ni
Raymond Goodison, ambao walikamatwa walipotaka kupanda treni kutoka uwanja wa ndege wa Gatwick kuelekea Victoria ndani ya London.
Wakati Polisi wakifanya ukaguzi
waligundua kilo moja ya cocaine yenye thamani ya dola £180,000 zikiwa
imeshonewa kwenye sidiria ya mwanamke huyo.
Nola
anasubiri kifungo chake, huku kijana aliyeambatana naye amehukumiwa
kifungo cha miaka 13 kwa kosa la kujaribu kuingiza zaidi ya kilo moja ya
dawa za kulevya aina ya Cocaine huku ikibainika kuwa sio tukio lake la
mara ya kwanza.

watuhumiwa wa dawa za kulevya.
No comments:
Post a Comment