08 January 2015

PICHA: HUYU NDIYE BINTI MDOGO ALIYEWEKWA KWENYE REKODI YA DUNIA KWA KUFANYA HIKI..!

Zu 
Unapokuwa karibu na mtoto wako na kumfuatilia ni rahisi kujua kipaji chake na kukiendeleza ingawa ni wazazi wachache wanaoweza kufanya hivyo, msichana kutoka Nigeria ambaye anasoma Marekani anakuwa msichana mdogo aliyeweza kuvunja rekodi kadhaa kubwa duniani.
Zuriel Oduwole, umri wake ni miaka 12, ameweka historia nyingine baada ya documentary yake ya ‘A Promising Africa’ kuwa documentary ya binti mdogo zaidi duniani kuonyeshwa katika majumba makubwa ya cinema.
Jarida la Forbes lilimtaja kuwa msichana mdogo mwenye asili ya Afrika ambaye ni miongoni mwa watu 100 mashuhuri wenye ushawishi zaidi Afrika waliotajwa kwa mwaka 2013 wakiwemo Marais watatu, pia akawa na rekodi ya kuwa mtu mdogo zaidi dunia kuandikwa historia yake katika Jarida la Forbes.
Documentary hiyo itaonyeshwa London, Januari mwaka huu na baadaye itaanza kuuzwa.
zuriel-and-kunle-afolayan-450x600

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname