NYOTA wa muziki wa Bongo Fleva, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ anadaiwa
kumpiga paparazi (wa blogu moja maarufu) kwa madai ya kuwa aliwahi
kumpiga picha akiwa mahakamani kipindi alipokamatwa na dawa za kulevya.
‘Chid Benz’ akiwa mahakamani kipindi alipokamatwa na dawa za kulevya.
Tukio hilo lilitokea Jumapili katika Ukumbi wa Maisha Club, jijini
Dar, ambapo Kundi la Yamoto Band walikuwa wakizindua wimbo wao mpya wa
Itanipwelepweta, Chid Benz naye alikuwepo maeneo hayo na baada ya shoo
alifuatwa na baadhi ya mapaparazi kwa ajili ya mahojiano.
Akizungumza na gazeti hili paparazi huyo alisema kitendo cha
mapaparazi kukusanyika mbele yake Chid alionekana kukumbuka kitu na
kuanza kumpiga vibao.
“Alipomaliza kunipiga vibao alitoka nje na kuwaita watu waje
wanipige, wameniumiza sana mbali na kujitetea waliendelea kunipiga mpaka
pale alipokuja Babu Tale kuamua ndipo ugomvi ukahamia kwake na Chid
akaanza kuvua fulana, cheni na kumpa mtu amshikie na kutaka kupigana na
Babu Tale tena,” alisema.
Gazeti hili lilimtafuta Babu Tale na baada ya kusikia madai hayo
alikana na kusema hataki kuhusishwa na ugomvi huo na mpaka gazeti
linaenda mtamboni Chid alikuwa hapatikani hewani.
No comments:
Post a Comment