Siku za sikukuu za Christmas na Mwaka mpya ni siku ambazo watu mbalimbali ulimwenguni kote hujumuika kwa pamoja kwa ajili ya kusherekea kuzaliwa kwa Yesu kristo na mwaka mpya kwa ajili ya kumaliza mwaka na kuukaribisha mwaka mpya.
Viongozi wa dini husisitiza wakristo wote duniani kuungana kwa pamoja kumwabudu mwenyezi Mungu kwa kutenda matendo yanayo mpendeza mwenyezi mungu ikiwemo kusaidia wasio jiweza kutenda matendo mema.
Aidha, kinachoshangazwa katika sikukuu hizi waumini wa kikristo pamoja na madhehebu mengine badala ya kumwabudu Mwenyezi Mungu wa mbinguni siku hizi zimekuwa zikitumika kuongeza maambukizi ya magonjwa ya zinaa ukiwemo ugonjwa wa UKIMWI.
Watu wengi siku hizi muhimu huzini pasipo kumuogopa mwenyezi Mungu. Ndoa nyingi huingia katika migogoro na kupelekea nyingine hata kuvunjika. Hata nyumba za kulala wageni (guest house ) hujaa sana watu suala linalothibisha kwamba asilimia kubwa ya watu hutumia siku hizo kuzini.
Watu wengine hunywa pombe kupita kiasi na kutoa lugha za matusi, Kuendesha magari wakiwa wamelewa suala linalopelekea ajali na pengine ajali hizo kusababisha vifo. Uhalifu nao unaongezeka katika siku hizi muhimu.
Biblia inasemaje kuhusu siku za sikukuu ?
Vitabu vya Mungu vinasisitiza watu kusherehekea sikukuu za Kristmasi na mwaka mpya kwa amani na kwa kutenda matendo mema yanayo mpendeza mwenyezi mungu.
…………………… Kheri ya Christmas na Mwaka Mpya………………
No comments:
Post a Comment