Rapper Mabeste ameeleza kwa urefu jinsi mke wake alivyougua kwa muda mrefu mara tu baada ya kujifungua mtoto wao wa kwanza, Kendrick.
Mabeste amesema mke wake ambaye pia ndio meneja wake alizidiwa hadi ikafika wakati akahisi atampoteza.
Kupitia Instagram, hivi ndivyo alivyoandika:
“Wabongo hawakosi cha kusema! Okay its true my fans nime wa promise sana juu ya ngoma mpya, mom & dad tv show, then kimya kimekua kingi! Ukweli wa ukimya wangu huu hapa!! Tangia nitoke bhits managers wamejitokeza weng sana but kiukweli asilimia 90 yao niligundua wanataka kunitumia tu….so mwisho siku nikaona bora mke wangu ndo awe Manager wangu coz itani protect!! She is very good …hard work,creative,hustler,respectful ana kila sababu ya kua manager wangu! Hata baadhi ya wasanii wenzangu ambao wanamfaham my wife wanajua hilo.
So hizi ni rumors zinazo sambaa kua my wife kanipoteza kwenye game! Ukweli ambao sijawai usema nimeuficha kwa mda mrefu ni huu wife wangu ameumwa mda mrefu sana ever since kajifungua my son hakua sawa….then hali ikawa mbaya zaid five months ago! So I had to be there for her,ilifikia stage nikahis I will loose her! I lost my mom nikiwa mdogo I didn’t want the same for my son….mda mwingi nimeutumia kumuuguza my wife na kucheer na mtoto wangu!! Hapo awali nlikua napost picha za wife nikisema get well soon na zingine nikiwa church!!
Nlitumia mda wangu kuuguza na nikishinda church kumuomba Mungu! So kazi zisingeweza kwenda hata kama ningekua Bhits au ningekua na manager mwingine!! Nilificha nikasingizia vngine but coz lies n rumors zmekua nyingi lemmi b open to my fans, now Mungu amejibu maombi yuko poa sana! Kuna sister mmoja wa clouds mwaija alishuhudia my wife alivyoteseka!! Wasaniii wenzangu wachache ambao ni friends wa wife, godzilla,young D,quick racka, cyrill , hemed phd etc: wanajua lisa a.k.a mama teen ni creative hustler, na kabla ya kua na mabeste alikua anafanya projects zake na hao artist nilio wataja walikua waki mpa support!!
Pia mtu mwenye akili zake akiangalia interview yangu na Bhits ambayo iko YouTube utajua tuu she is more that!! Events zangu zote wife ndo alizi plan! Behind every successful Men there is a woman!! Nisiongee sana kapona acha tuone 2015! Mlio dhani mabeste kaishiwa mimi mwenzenu ndo kwanza safari inaanza.”
No comments:
Post a Comment