Wakati
Dunia ikipinga vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na
watoto hapa nchini Bado vitendo hivyo vimeonekana vikiendeleea ambapo
MTOTO Mmoja BENSON TOLE mwenye umri wa miaka Mitano mkazi wa Ruhuwiko
mjini Songea mkoani Ruvuma, amenusurika kifo baada ya kukatwakatwa kwa
kitu chenye ncha kali sehemu za usoni na Mzee mmoja LONGINUS HAULE
mwenye miaka 51 akimtuhumu mtoto huyo kumuibia
matunda aina ya Mapera shambani kwake.
EMMANUEL MSIGWA kutoka mjini Songea
Mtoto BENSON TOLE kwa sasa amelazwa katika hospitali ya mkoa mjini
Songea katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU), Madaktari wanaendelea
kunusuru uhai wa mtoto huyu baada ya kupata mashambulio makali ya
kucharangwacharangwa na kitu chenye ncha kali sehemu za usoni na
mtuhumiwa mmoja LONGINUS HAULE mkazi wa Polisi Lizaboni mjini Songea.
Mzee HAULE anatuhumiwa baada ya kumfanyia unyama wa kutosha mtoto
huyo na kisha kupoteza fahamu akimtuhumu kumuibia matunda aina ya mapera
shambani kwake alimtupia kwenye nyumba moja ambayo haijaisha ujenzi
wake akidhani tayari ameshamuua.
Afisa Muuguzi wa Hospitali ya mkoa mjini Songea, JOSEPH MTEWELE amesema
kwa sasa mtoto huyo yupo chini ya uangalizi maalumu na kwamba madaktari
wanaendelea na jitihada za kunusuru uhai wake kutokana na majeraha
makubwa aliyoyapata sehemu za kichwani.
Jeshi la polisi mkoani Ruvuma limetihibitisha kutokea kwa tukio hilo
na kwamba linaendelea kuchukua hatua zaidi za kumfikisha Mzee LONGINUS
HAULE kwenye vyombo vya sheria kwa hatua zaidi.
No comments:
Post a Comment