STAA wa filamu Bongo, Rose Ndauka ameanika ukweli kuhusu uhusiano wake na aliyekuwa
mchumba wake Malick Bandawe baada ya kuwagundua wanawake wawili aliozaa
nao mbali na yeye.Staa wa filamu Bongo, Rose Ndauka.Kwa mujibu wa
chanzo chetu, Rose aliamua
kufungasha virago vyake na kurudi kwa mama yake mzazi maeneo ya Kigogo
baada ya kugundua kwamba mchumba’ake huyo alizaa na wanawake wawili
tofauti na yeye ambaye ni wa tatu. “Alichokizungumza Malick kwamba
alishamuweka chini Rose na kuzungumza naye si kweli, ila yeye Rose
aliamua kurudi kwao baada ya kugundua jamaa ana wanawake wawili aliozaa
nao kabla yake,” kilisema chanzo hicho.
Akaongeza: “Kile kilichosemwa na Malick kuwa anasikitika kuona mtoto wake anakwenda kulelewa na mwanaume mwingine ni kujitetea tu lakini ukweli ni kwamba mwanaye analelewa na yeye mwenyewe kwa sababu yuko nyumbani kwa mama yeke.”
Juzi, paparazi wetu alimtafuta Rose kwa njia ya simu yake ya mkononi,
alipopatikana na kusomewa madai hayo alikata simu huku akisikika
akisema hayuko tayari kufunguka lolote kwa sasa
No comments:
Post a Comment