03 October 2014

HATIMAYE MTITU AFUNGUKIA BIFU LAKE NA STEVE NYERERE!

BAADA ya tetesi kuzagaa kwamba aliyekuwa Katibu wa Bongo Movie Unity, William Mtitu kwamba ana bifu kali na aliyekuwa mwenyekiti wa kundi hilo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ mwenyewe amefunguka kwamba hawezi kufanya kitu kama hicho.Aliyekuwa Katibu wa Bongo Movie Unity, William Mtitu.
Akistorisha na paparazi wetu, Mtitu amesema anashangazwa na taarifa hizo licha ya kwamba hawajawahi kuzungumza na Steve tangu alipoachia ngazi ya ukatibu.
“Sijawahi kutishia kuua mtu kama watu wanavyosema, Steve ni mdogo wangu hivyo kama atakuwa na bifu na mimi ni yeye na sitajali kwani wangekuwa ni kina Ray au wasanii wengine wakubwa wamenichunia ningewaza lakini huyo haniumizi kichwa,” alisema

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname