03 October 2014

BINTI MDOGO APONZWA NA UZURI WAKE, ACHARANGWA VITU NA MABINTI WENZAKE KISA WIVU!


Binti mdogo wa miaka 15 raia wa Argentina Julia Alvarez amepatwa na majanga yaliyomfanya apoteze muonekano wake mzuri baada ya mabinti wawili wenye wivu kumcharanga uso wake kwa visu kisa uzuri wake uliopitiliza! 
Julia anasema alikuwa anatembea kurudi nyumbani akitokea mji wa Juan Domingo Peron huko northern Argentinian ndipo wasichana hao wawili mmoja ana miaka 18 na mwingine 16 walipomvaa bila huruma. 
"Kila mtu anasema wewe ni mzuri sana..huwezi kuonekena mzuri tena tukishamalizana na wewe hapa..na watu watakuita majina mabaya'' Julia alisema haya ni maneno aliyoambiwa kabla ya kucharangwa visu usoni. 

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname