02 October 2014

KIMENUKA MBAYA: MATUSI YAMPONZA MAMA WEMA SEPETU...KAJALA AAMUA KUJIBU MAPIGO



 Habari ya mjini kwa sasa ni bethidei ya Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu kutimiza miaka 26 tangu kuzaliwa, lakini ndani ya tukio hilo, mengine yameibuka! 
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Kajala Masanja. Miongoni mwa yaliyoibuka kwenye sherehe hiyo iliyofanyika Jumapili iliyopita nyumbani kwa Wema, Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar es Salaam ni madai ya mama Wema, Mariam Sepetu kudaiwa kupewa nafasi ya kutoa ‘neno la hekima’ lakini akaitumia kumvurumishia mitusi aliyekuwa shosti wa Wema, Kajala Masanja. 
Baada ya sherehe hiyo, Jumatatu na Jumanne, mitandao mingi ya kijamii ilitumbukiza video yenye sauti ikimuonesha mama Wema akimrushia matusi Kajala kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutokana na kukorofishana kwa mwanaye na Kajala aliyewahi kumfadhili mahakamani kwa kumlipia faini ya shilingi milioni 13 asiende jela kwa kesi ya kuuza nyumba iliyokuwa na zuio la kisheria.


Wema Sepetu akiwa na mama yake. KAJALA AAMUA ZITO

Katika kufuatilia sakata hilo, Amani lilinyetishiwa kwamba Kajala baada ya kushindwa kuvumilia, ameamua kumshitaki mahakamani mama Wema. Chanzo chetu kinadai kuwa Kajala alifikia uamuzi huo baada ya kushauriwa na familia sanjari na wafuasi wake (Timu Kajala) ambapo sasa, timu hiyo na Timu Wema wameingia vitani tena.BOFYA KUSOMA ZAIDI>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname