Habari ya mjini kwa sasa ni bethidei ya
Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu kutimiza miaka 26 tangu kuzaliwa, lakini
ndani ya tukio hilo, mengine yameibuka!
Miongoni mwa yaliyoibuka kwenye sherehe
hiyo iliyofanyika Jumapili iliyopita nyumbani kwa Wema, Mtaa wa Bwawani,
Kijitonyama jijini Dar es Salaam ni madai ya mama Wema, Mariam Sepetu
kudaiwa kupewa nafasi ya kutoa ‘neno la hekima’ lakini akaitumia
kumvurumishia mitusi aliyekuwa shosti wa Wema, Kajala Masanja.
Baada ya sherehe hiyo, Jumatatu na
Jumanne, mitandao mingi ya kijamii ilitumbukiza video yenye sauti
ikimuonesha mama Wema akimrushia matusi Kajala kwa kile kilichodaiwa
kuwa ni kutokana na kukorofishana kwa mwanaye na Kajala aliyewahi
kumfadhili mahakamani kwa kumlipia faini ya shilingi milioni 13 asiende
jela kwa kesi ya kuuza nyumba iliyokuwa na zuio la kisheria.
Katika kufuatilia sakata hilo, Amani
lilinyetishiwa kwamba Kajala baada ya kushindwa kuvumilia, ameamua
kumshitaki mahakamani mama Wema.
Chanzo chetu kinadai kuwa Kajala
alifikia uamuzi huo baada ya kushauriwa na familia sanjari na wafuasi
wake (Timu Kajala) ambapo sasa, timu hiyo na Timu Wema wameingia vitani
tena.
“Kajala
ameshawasiliana na wanasheria wawili na kutoa maelezo yake, wao
wanaandaa faili ili mashitaka yafike mahakamani, amekasirika sana.
“Amesema mama Wema ametumia nafasi ya kukutana na watu kumdhalilisha bila kumpa nafasi ya kujitetea, ameona si sawa hata kidogo,” kilisema chanzo hicho ambacho ni jirani na Kajala.
“Amesema mama Wema ametumia nafasi ya kukutana na watu kumdhalilisha bila kumpa nafasi ya kujitetea, ameona si sawa hata kidogo,” kilisema chanzo hicho ambacho ni jirani na Kajala.
Katika sauti, mama Wema anasikika
akitamka matusi (hayaandikiki) huku Wema naye anasikika akimsihi mama
yake asimtaje jina Kajala kwa kuwa kufanya hivyo ni kumpaisha. Hapa
inamaanisha kwamba, Wema alitaka mama yake afunguke lakini bila kutamka
jina la mtu.
Katika hatua nyingine, mama Wema alisema
kauli iliyoashiria kwamba Timu Kajala ilikuwemo ndani ya bethidei ya
mwanaye. “Nasema haya huku najua humu ndani kuna Timu Kajala, lakini
nasema….(matusi mazito)”
Baada ya madai hayo yote, juzi, Amani
lilimsaka Kajala kwa njia ya simu ili kumuuliza ukweli wa madai hayo.
Licha ya kutopokea simu ya mwandishi wetu, alitumiwa ujumbe mfupi wa
maneno ‘SMS’ na kuulizwa kila kitu.
Hata hivyo, badala ya kujibu alikaa
kimya, baada ya dakika kama kumi na tano alimrushia kwa simu mwandishi
wetu video hiyo ambayo anadai kutukanwa na mama Wema bila kusema
chochote hali iliyotafsiriwa kuwa kama alisema; ‘hebu oneni wenyewe
jamani, nimemkosea nini mama Wema?’
Katika hatua nyingine siku hiyo, meneja
wa Wema, Martin Kadinda alikuwa na kazi ya ziada kuhakikisha, mama Wema
na mama Diamond, Sanura Kasim ‘Sandra’ hawakai jirani au meza moja licha
ya kwamba watoto wao wamependana.
“Kadinda ana kazi ngumu sana, unajua
anatakiwa kuhakikisha kwamba mama Wema na mama Diamond hawakai meza
moja. Sijui anaogopa nini, kwani hawa si watu ambao watoto wao wana
mpango wa kuoana?” alihoji mwalikwa mmoja.
Katika bethidei hiyo, Wema alizawadiwa
magari mawili, Nissan Murano lenye thamani ya shilingi milioni 36
alilopewa na Diamond na BMW 545i lenye thamani ya shilingi milioni 56,
inadaiwa alizawadiwa na Kadinda!
No comments:
Post a Comment