MSANII
mkongwe wa filamu Ummy Wenslaus ‘Dokii’ amemkabidhi swahiba wake Lucy
Komba, kiwanja chenye ukubwa wa robo hekari, kilichopo Bagamoyo mkoani
Pwani, tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita, ikiwa ni
kutekeleza ahadi aliyoitoa kwenye kicheni pati yake.Msanii mkongwe wa
filamu Ummy Wenslaus ‘Dokii’. “Mimi naona tunaendana kitabia na Lucy,
alinipa kazi moja katika filamu yake ya Yolanda nikiwa kwenye kipindi
kigumu sana, hivyo ni rafiki yangu wa kweli maana wengine wanaogopa hata
kunishirikisha kwenye kazi zao wanajua nitawafunika,” alisema Dokii.
Msanii
mkongwe wa filamu Lucy Komba akiwa na mume wake Stanley.Kwa upande wa
Lucy alisema: “Mimi sijawahi kuona urafiki wa namna hii, maana wengine
wanatunzana hela kwenye kumbi kitu ambacho siyo sahihi, lakini nashukuru
Dokii kanipa kitu ambacho naweza kujivunia maisha yangu yote mpaka
wajukuu zangu.”
No comments:
Post a Comment