Madee
alikamatwa na Polisi saa kadhaa zilizopita baada ya tukio la yeye
kuibiwa simu akiwa kwenye gari tena likitembea ambapo waliohusika ni
watu wawili wakiwa kwenye pikipiki saa tisa usiku akitoka Kigamboni Dar
es alaam kufanya show hivyo akawa anavuka bahari ili aelekee nyumbani.
Baada ya kuchoropoa hiyo simu jamaa wa pikipiki walianza kukimbia
hivyo na dereva wa Madee akaanza kukimbizana nao na kufanikiwa kuwagonga
alafu pikipiki ikaanguka ila jamaa wa nyuma aliechoropoa simu
akafanikiwa kukimbia ila yule aliekua anaendesha wakambeba na kwenda nae
maskani Tiptop kwa lengo la kumuhoji ili wampate aliekimbia na simu.
Kilichomfanya Madee akamatwe na kuwekwa Polisi ni madai yake kwamba
kesi hiyo imegeuzwa na sasa yeye ndio anaonekana mwenye makosa kwa
kumteka huyu jamaa waliekwenda nae Tiptop Manzese.
Haya ndio mambo 10 anayoyasema Madee.
1. Nilikaa Polisi kwa zaidi ya saa 32, nililala na kuamkia huko.
2. Kule ndani
haupo huru ndio maana kuna mateso, unapangiwa muda wa kulala na
hautakiwi kuongea kwa sauti kubwa… mle ndani watu wanatolewa njee saa
moja usiku tunahesabiwa pale nje alafu mkishaingizwa ndani kimyaaaa.
3. Kwenye room
niliyoshikiliwa nilikua na watu kama 30 hivi ila sijui kwenye room
nyigine ya pili sijui kulikua na watu wangapi sababu sikuingia.
4. Nilianza kushangiliwa
nilipotokeza tu pale kwa juu wakati naingizwa machizi waliponiona mimi
wakaanza kuimba ule wimbo wangu wa ‘majuto ni mjukuu‘ niliozungumzia ishu za Polisi.
5. Nilivyofika
kule nilikuta kumejaa ila kumbe kuna sehemu tayari nilishawekewa na
machizi sehemu poa tu upepo unaingia fresh tu sema ndio hivyo mazoea
mazoea tu huwezi kulala….
6. Mle ndani
hakuna vitanda zaidi ya sakafu tu nilitamani hata nijaribu kupeleka
maombi niwapelekee machizi mikeka kidogo wawe wanalalia.
7.
Nilisimamishwa Mahakamani September 25 kwa mara ya kwanza sababu jamaa
wamejaribu kutengeneza vitu vingine viwili tofauti na ilivyokua,
wanasema mimi nimemteka mtu na pikipiki yake nikaenda kumjeruhi na
washkaji zangu ila ukweli ni kwamba huyu jamaa alikua na rafiki yake
kwenye pikipiki wakanipora simu yangu wakati nikiwa nimekaa kwenye gari.
8. Baada ya
hapo dereva wangu mtundu akakimbia akaiblock pikipiki na kuigonga
wakaanguka lakini yule aliekua amechukua simu akakimbia ila aliekua
anaendesha tukamkamata tukampakiza kwenye gari na kuondoka nae mpaka
maskani ya Tiptop ila nikampigia simu mama yake nikamwambia mwanao yuko
hapa njoo uongee nae aturudishie simu yetu.
9. Mama yake
alikuja akaondoka na kusema anakwenda kumtafuta aliechukua simu lakini
cha kushangaza Mama asubuhi akaja na Polisi wakamchukua jamaa na
kumpeleka Magomeni wakati huo mi nilikua nimekwenda Mwanza kwenye show.
10. Niliporudi
kutoka Mwanza nikakimbilia Polisi Magomeni kwenda kuulizia napataje haki
yangu nikaambiwa hili shauri linahamishiwa Kigamboni, nilipokwenda
Kigamboni Polisi nikakuta hiyo kesi kwamba Madee kamteka mtu nikawekwa
ndani, hii ni kama mara yangu ya nne au ya tatu nawekwa Polisi…. hizo
nyingine zilishatokea zamani ambapo ya mwisho ilikua miaka sita au saba
nyuma, hii kesi ya sasa ipo Mahakamani.
No comments:
Post a Comment