Baadhi ya watafiti wana sahuku ikiwa vipimo vya sketi vitamtahadharisha mwanamke kuhusu tisho la Saratani
Utafiti unaonyesha kuwa wanawake wanaonenepa maishani bila ya kuwa waangalifu wanajiweka katika hatari ya kupata Saratani.
Watafiti
kutoka chuo Kikuu cha London wanasema kwamba wanawake walio kati ya umri
wa miaka 24-28 ambao huendelea kunenepa kila baada ya miaka 10, wako
katika hatari zaidi ya kupata Saratani ya Matiti baada ya kupitisha umri
wa kuzaa.
Sasa je
ni nini ishara ya mwanamke kunenepa? Watafiti wanasema vipimo vya sketi
yake vinaweza kukusaidia kujua ikiwa uko katika hatari ya kpatwa Saratni
ya Matiti au la.
Kila
unapogundua kuwa sketi yako inaendelea kuwa ndogo kiunoni, basi
inakubidi ujue kuwa mwili wako unaongekeza kwa unene. Na pia ni rahisi
kwa wanawake kukumbuka kipimo cha sketi kuliko kitu kingine chochote.
Kwa hilo
watafaiti wanasema mwanampe anapaswa kutahadhari kila sketi yake
inapoendelea kuwa ndogo kwake maana kwamba amenenepa zaidi. Ikiwa ukubwa
wake unazidi kwa kipimo cha sketi mbili katika kipindi kimoja basi
mwanamke anakuwa katika hatari ya kupatwa na Saratani hata zaidi.
'Mfumo wa maisha
No comments:
Post a Comment