WATU
wawili akiwamo askari mmoja wamenusurika kifo baada ya kupigwa risasi
na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, waliofanikiwa kupora mfuko wa
fedha unaosadikiwa kuwa na zaidi ya shilingi milioni 30.
Tukio
hilo, lilitokea jana mchana majira ya 8:30 katika Mtaaa wa Mlandege
Mkoa wa Mjini Magharibi, ambapo majambazi hao walimvamia mmoja wa
wafanya biashara wa Mchele hapa nchini aliyetambulika kwa jina la Salum
Issa Suleiman (50), Mkaazi wa Baghani Mjini Unguja, ambaye walimpora
mfuko wake wa fedha hizo wakati akiwa njiani kuzipeleka benki.
Wakati tukio hilo
likitokea mmoja wa askari polisi wa Kituo cha Malindi Sajenti Hija
Hassan Hija, alijaribu kupambana namabambazi hao, lakini alishindwa
kufanikiwa baada na yeye kujeruhiwa sehemu ya mkononi na mguuni kutokana
kushambuliwa kwa risasi.
Mfanyabiashara
Salum alisema wakati alipokuwa akielekea maeneo ya Benki hiyo ndipo
ilipotokea gari ndogo mbele yake na kumnadia mwizi na hapo ndipo
walipompiga risasi ya mguu wa kulia na kumnyang’anya fedha hizo na
kuondoka nazo.
Kwa
upande wake askari Hija alisema, alipofika maeneo hayo ndipo alipomkuta
Mfanyabiashara huyo akiwa katika harakati za kujinasua na hali na ndipo
askari huyo alipokwenda kumuokoa lakini na yeye alishambuliwa na
majambazi hao na kufanikiwa kuondoka na kitita hicho cha fedha
zamfanyabiashara huyo.
Hata
hivyo, majeruhi hao bado wanaendelea kupata matibabu katika Hospitali
kuu ya Mnazi mmoja na hali zao walieleza kuwa zinaendelea vizuri.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi,
Mkadam Khamis Mkadam, alisema ni kweli tukio hilo limetokea na
aliyeporwa fedha hizo ni Mfanyabiashara wa Mchele katika maeneo ya
Bandarini ambae alikuwa akielekea katika Benki ya PBZ tawi la Mlandege.
Alisema
mfanyabiashara huyo alikuwa na fedha zenye thamani ya shilling milioni
30,6,00,000, ambazo ni mali ya tajiri wake anafahamika kwa jina la
Yussuf Mohamed, ambazo alikuwa anakwenda kuziweka katika Benki hiyo.
Hata
hivyo, Kamanda Mkadam, alitoa wito kwa Wananchi wakati wanapokwenda
kuweka pesa kuacha kwenda kwa miguu na kuwatumia askari kwani askari
wapo kwa ajili yao ili kuimarisha usalama wa raia.
Taarifa ya Tatu Makame, Laylat Khalfan
No comments:
Post a Comment