26 August 2014

NESI MUHIMBILI AKATWA MIGUU

Flora Nathaniel Shayo akatwa miguu baada ya kuugua kisukari.

Flora Nathaniel Shayo (60) mkazi wa Chanika, wilayani Ilala, Dar ameiomba serikali pamoja na Rais Jakaya Mrisho Kikwete imsaidie baada ya kukatwa miguu kutokana na kuugua ugonjwa wa kisukari.

Akizungumza na waandishi wetu hivi karibuni, Flora alisema aliwahi kuwa muuguzi (nesi) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa miaka 26 iliyopita na baada ya kustaafu alikuwa akifanya biashara ya kuuza dawa za binadamu (Duka la dawa) huku mwanaye akiwa anafanya kazi za muziki. Mama huyo aliendelea kufunguka kuwa, aligundulika kuwa na ugonjwa wa kisukari na presha mwaka 2006 ndipo akaanza kutumia dawa. 


CHANZO CHA UGONJWA
Akifafanua zaidi mama huyo alikuwa na haya ya kusema: “Mwaka 2011 kidole gumba cha mguu wangu wa kulia kilianza kukauka na kubadilika rangi nikaenda Hospitali ya Taifa Muhimbili. 
“Nilipofika hospitali nilipimwa na kugundulika kuwa sumu imepanda mpaka juu karibu na goti, madaktari wakaniambia ni lazima nikatwe mguu ili kuokoa maisha yangu. Nilipatwa na woga, lakini sikuwa na la kufanya, nilikubali. SOMA ZAIDI>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname