MWANAFUNZI wa Chuo cha Uuguzi Chimala wilayani Mbarali, Mkoa wa Mbeya, Vena Mtati (27) (pichani) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa kwa madai mazito ya kumuua mtoto wake kwa kumnyonga, kumtumbukiza kwenye mfuko wa rambo na kuutia ndani ya mfuko wa salfeti kisha kuuficha chini ya kitanda!
Tukio hilo la kikatili ambalo limewashangaza wengi, hasa ikizingatiwa kuwa mtuhumiwa huyo anajua sheria kwa sababu anajifunza uuguzi, lilijiri Agosti 21, mwaka huu ndani ya nyumba moja iliyopo Kijiweni, Kata ya Mvinjeni mjini hapa.
SHUHUDA
Kwa mujibu wa shuhuda ambaye anaishi jirani na nyumba inayodaiwa kufanyika mauaji hayo (jina lipo), wiki mbili zilizopita, mtuhumiwa huyo alifika kwenye nyumba hiyo akitokea chuoni akiwa na ujauzito. “Wiki mbili zilizopita, Vena alifikia kwa rafiki yake anayeitwa Joyce ambaye alikuwa amepangisha katika hiyo nyumba. Vena alikuwa na mimba kubwa, baada ya siku tano tu akajifungua,” kilisema chanzo hicho. SOMA ZAIDI>>

No comments:
Post a Comment